Tuesday, August 20, 2024

Jifunze ufugaji wa mnyama ndezi

 Kuna sababu ya kuanza kumfuga mnyama ndezi nchini Tanzania 

Haya ni mawazo ya mbena Riziki G, bachelor degree of rural development Sokoine university of Agriculture.

Blog hii imeanzishwa Kwa ajili ya kutoa elimu Kwa Jamii juu ya umuhimu wa kuanza kumfuga mnyama ndezi majumbani.

Ufugaji wa ndezi tanzania


Tukitafakari na kuchunguza vizuri kuku tunaowafuga Leo hapo zamani za kale walikuwa ndege wa porini.

Kanga au (guinea foul) mpaka Leo hii bado wapo porini na wengine tunawafuga majumbani.

Asilimia ya wanyama wote na ndege tunaowafuga majumbani asili Yao ilikuwa porini.

Ndezi ni aina ya mnyama ambae anatoweka, miaka ya 80 mpaka 90 vijiji vingi ndezi walikuwa wakifika Hadi majumbani kujitafutia chakula kama majani yaliyopo jirani kabisa na makazi ya binadamu au walisogea kula mazao yaliyopo karibu kabisa na makazi ya watu bila kuhofu kukamatwa na binadamu lakini miaka ya Leo ni nadra sana kumwona ndezi jirani na makazi ya watu. Na akionekana atawindwa mpaka awe kitoweo.

Ndezi ni mnyama anaependwa kuliwa na baadhi ya binadamu. Nyama yake ni tamu sana na Haina mafuta mengi. Nyama ya ndezi hukaushwa na kuliwa kama nyama choma au kuichemsha na kuiunga mchuzi Kwa kutumia karanga za kusagwa na ziwe zimekaangwa kabla ya kuzisanga na kuzikwangua ngozi nyekundu ya nje ya karanga na nyama ya ndezi huchemshwa  baada ya kuwa imekaushwa Kwa moto hafifu takribani masaa matatu Hadi sita.

Kutokana na sababu hizo Mr Mbena Riziki G aliamua kuanzisha project ya kufuga ndezi na kuelimisha jamii kuanza kufuga mnyama ndezi.

Mr mbena Riziki G alifanya observation Kwa kutumia mitandao ya kijamii Ili kujua uhitaji wa watu kupata kitoweo Cha nyama ya ndezi tanzania, alichapisha habari ya kuuza ndezi pale Facebook akiwa Hana ndezi hata mmoja na hakujua Wala sehemu ya kumpata ndezi wa kuanza kufuga Nia yake  Ilikuwa aone watu wanaichukuliaje nyama ya ndezi na mnyama ndezi Kwa ujumla majibu aliyopata watu zaidi ya 20 wali like post ya Facebook inayoelezea biashara ya ndezi na wengine walitoa maoni Yao kuwa wanatamani sana kupata nyama ya ndezi 

Unaweza soma maoni ya watu kwenye mtandao wa Facebook kupitia post link hizi:  Post 1: https://www.facebook.com/groups/633826251222732/permalink/1169688054303213/?app=fbl

Post 2: https://www.facebook.com/groups/633826251222732/permalink/1169688054303213/?app=fbl

Post 3: https://www.facebook.com/groups/1147383882284006/permalink/2206881893000861/?app=fbl


Post 4: https://www.facebook.com/groups/1147383882284006/permalink/2202287176793666/?app=fbl

Mwaka 2014 baadhi ya mitandao iliripoti habari ya ulaji na ufugaji wa ndezi Kwa Jina jingine kama cane rat au grass cutter ijulikanavyo nchi za maharibi mwa afrika kama Nigeria na Ghana, baadhi ya mitandao hiyo ni Jamii forums kwenye account yake ya Facebook unaweza kusoma kwenye link hii https://www.facebook.com/JamiiForums/photos/a.437622406301759/728330433897620/?type=3&app=fbl mitandao hiyo iliripoti habari ya ulaji na ufugaji wa ndezi baada ya chuo kikuu Cha kilimo Cha Sokoine kufanya utafiti na kugundua Kuna umuhimu wa kufuga na kula ndezi.

Mtandao wa mwananchi ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyoripoti habari hii ya ufugaji na ulaji wa ndezi Tanzania

Watanzania tule Nyama ya ndezi

Unaweza kusoma habari hii kwenye tovuti ya mwananchi https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/watanzania-kuleni-nyama-ya-panya-ina-vitamini-adimu-mwilini-2767244

Nchi za afrika maharibi kama Nigeria na Ghana mnyama ndezi anafugwa kibiashara na nyama ya ndezi inauzwa kwenye masoko kama nyama nyingine zililozoeleka.

Nyama ya ndezi ikiuzwa sokoni nchini Nigeria


Jinsi mchungaji nchini Ghana anavyotajirika Kwa ufugaji wa mnyama ndezi tazama video hii 


Weka  maoni yako kuhusiana na mradi wa kufuga ndezi Tanzania 

Comment hapa chini tutasoma maoni yako na kuyafanyia kazi.


0 comments: